RAPA Onika Tanya Maraj ‘Nicki Minaj’ huenda amenasa ujauzito kutoka kwa bwana wake mpya ambaye pia ni rapa, Nasir Jones ‘Nas’ baada ya kuposti picha ya ‘emoji’ ya mtoto mchanga.
Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa Twitter, Nicki aliposti picha ya emoji hiyo iliyoamsha hisia za mashabiki wengi huku wengine wakimpa ‘za chembe’ kuwa, badala ya kuachia wimbo mpya ndiyo kwanza anashika mimba. Hii si
mara ya kwanza kwa Nicki kuposti viashiria vya kunasa ujauzito, wiki mbili zilizopita aliandika maneno ya kuashiria kuwa mtoto wake yupo njiani kuja duniani. Mei mwaka huu, katika shoo ya The Ellen DeGeneres, Nicki alithibitisha kutoka na Nas na angependa kumzalia.
Source: Udaku