Bongo muziki unafanywa kienyeji” – Mwana FA

Rapa staa kutoka Bongoflevani Mwana FA amedai kuwa Bongo hakuna proper records label bali muziki unafanywa kienyeji enyeji mwishowe wasanii hubaki kutoleana kauli mbaya na mameneja wao.

Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM FA amesema anafikiria kuhusu Records Label lakini anasita kutoka na mifumo iliyopo ambapo kwa upande wake anaangalia namna ambavyo mfumo utaweza kuisaport.

“Ukiwa unafanya muziki kama unataka kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Maana yake unakuwa msanii mdogo, unakuja kuwa wa kati na baadaye unakuwa msanii mkubwa kabisa lakini the way muziki wetu ulivyokuwa setup hakuna hata proper records label bado.

“Ni kitu ambacho tunafanya kienyeji enyeji mwisho tutaishia kutukanana kama wasanii na mameneja wao wanavyotukanana. Ni kutu ninachokifikiria lakini kila watu kuna vitu vinanifanya nasita kidogo japo ni kitu kipo. Naangalia namna ambavyo huu mfumo wetu utaweza kuisaport.” – Mwana FA

Source: Millard ayo