Khaligraph Jones Anataka Cash.

Rapa kutoka nchini Kenya Brian Robert Ouko a.k.a Khaligraph Jones baada ya kudondosha video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa kwa jina ‘Nataka iyo Doh’ amesikika akikataa malipo ya mfumo wa cheki akiwa na Staa wa ngoma ya Korero ‘QBoy Msafi’.

Khaligraph katika ujio wa ngoma yake hiyo ambayo zaidi amezungumzia kulipwa pesa yake, yaani alipwe kwa kila atakachofanya, anasikika katika ngoma akisema ‘ akisema kuwa anahitaji malipo ya pesa halali mkononi na sio mfumo wa cheki huku akionekana kurusha rusha pesa katika kifaa cha cha kisasa cha msalani katika video ya wimbo huo.

“Nataka hiyo Pesa yangu Manzeee…Sitaki mambo ya deni hapa hivi, sitaki cheque…nataka cash money brooo…Nipatie hiyo pesa bro…” Ameseikika Khaligraph Jones.

Kutokea kwa QBoy katika video ya wimbo huu inaweza kuhisiwa kuwa katika hatua za kukamilisha video ya ‘Karorero Remix’ ambayo alimshirikisha Nai Boi wa nchini Kenya ndo kipindi ambacho ilishootiwa video hii ya Khaligraph.

Source: Dizzim Online.