Mkutano Uliofanyika Shule ya Lucky Vicent Polisi Waingilia

Leo May 18 kwenye shule ya Lucky Vicent Arusha, Polisi walivamia mkutano ulioongozwa na Meya wa jiji hilo akiambatana na viongozi wa dini, Madiwani na Waandishi wa habari ambao Meya alidai lengo lake ni kukabidhi rambirambi walizozichanga wao kutokana na msiba wa ajali ya Wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent.

Wakati viongozi hao wakiendelea kuhojiwa na Polisi Arusha, millardayo.com na AyoTV zinakukutanisha na video ya sehemu ya vilivyokua vinazungumzwa ndani ya mkutano huo kabla ya Polisi kuvamia.

Hii video hapa chini Katibu wa chama cha Wamiliki wa Shule binafsi mkoa wa Arusha Leonard Mao alikua anaongea >>> “Nilitangaza kwa niaba ya Watanzania siku ya kuaga ile miili 35 kwamba tutaendelea kuchanga rambirambi zetu na kwenda kuwaona wale wazazi mmoja baada ya mwingine“

“Hakuna hata senti ya mtu itakwenda pembeni…. hatumpi mtu hata kwenye shule ya Vicent, ni waliofiwa wenyewe mkono kwa mkono’

Source: Millard Ayo