Amini kayaongea haya kuhusiana na ukimya wake.

Mwimbaji staa zao la THT Amini amefunguka akisema sababu za yeye kukaa kimya kwa muda mrefu ni kuandaa vitu vizuri licha ya watu wengi kudai ukimya wake unasababishwa na ndoa kitu kinachotokea kwa wasanii kutokufanya vizuri kwenye muziki baada ya ndoa.

Kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM. Amini amesema kuwa ukimya wake hautokani na ndoa bali ni kwa lengo la kuandaa vitu vizuri ili asiwe anasita kutoa nyimbo akidai kuwa tayari ana nyimbo zaidi ya 10 ambazo anajiandaa kuziachia.

>>>“Kuwa kimya kwangu sio kwa sabbau ya kuoa ila mimi napenda kuandaa vitu vizuri ili vitu ninavyovitoa nisiwe nasitasita wakati naziachia. Kwa hiyo kwa sasa hivi nipo naandaa nyimbo nyingi ili ninaavyoanza kutoa nyimbo inakuwa nonstop. Kwa ngoma amabazo zipo tayari kwa kutoka zipo kama Kumi.

“Sikuwa na nia ya kusuka albamu, nilikuwa naandaa single kwa ajili ya kwenda kutikisa ulimwengu. Kwa hiyo, kama kutakuwa na mtu atajitokeza kutaka albamu ya Amini basi nitasuka nyimbo zote kwenye hiyo albamu.” – Amin

Source: Millard ayo