Dogo Janja aitaja My life kuwa ngoma yenye sauti nyingi.

Msanii wa muziki wa kizazi toka Tip Top Connection ‘Dogo Janja’ amezungumzia mfumo wake wa kuhusisha wasanii wengi kuingiza sauti katika nyimbo zake kama njia ya kuongoza uhondo katika ngoma zake.

Akizungumza na Dizzim Online, Janja amesema kuwa mfumo huo sio mpya sana kwa wafatiliaji wa muziki hasa kusema kuwa unafanyka sana kwa wastaa marufu duniani na kuitaja ngoma yake ya ‘My life’ kama ngoma iliyohusisha wanasii wengi katika kuogeza sauti ambazo ziliongeza ladha zaidi.

“Kati ya ngoa zangu ambazo zimeongezwa sauti na wasnii wengi ni My life, kuna Madee, Kuna Dully Sykes, Mimi na Producer” Amesema Dogo Janja.

Hata hivyo Dogo Janja anengeza kusema kuwa hana msanii yoyote anaye mpa changamoto zaidi yake mwenye kwakuwa muziki wake umekua sana kwa kiasi kikubwa hasa katika ongezeko la ubunifu na mabadiliko ya miondoko ya kizazi kipya zaidi.

Source: Dizzimonline