chembe za protini za maziwa ya Mende zina virutubisho vingi ajabu.

WENGI huenda wakawa hawawezi kuwavumilia Mende, hata kwa kuwatazama tu, lakini wanasayansi nchini India wanasema huenda Mende wakatoa tumaini kwa binadamu, katika suala zima la lishe.
Wanasayansi hao wamegundua kwamba chembe za protini za maziwa ya Mende zina virutubisho vingi ajabu.
Wanabainisha kuwa chembe hizo zinaweza kutumiwa kama tembe ama chakula chenye virutubisho vya protini kwa kiwango cha juu.
Wanasayansi hao ambao wanatoka kwenye Taasisi ya Sayansi ya Seli katika mji wa Bengaluru, wamefanya ugunduzi huo baada ya kutafiti muundo wa chembe za protini zinazopatikana katika utumbo wa aina ya Mende wajulikanao kama Diploptera puncata, ambao ndio aina pekee ya mdudu huyo inayojifungua.
Ingawa Mende wengi kwa kawaida hawatoi maziwa, Mende aina ya Diploptera puncata huwa wanatengeneza aina fulani ya maziwa yenye protini kwenye utumbo, ambayo hutumiwa kulisha watoto wao.
Chembe moja ya protini hiyo inakadiriwa kuwa na kiwango mara tatu cha nguvu ya mwili ikilinganishwa na kiasi sawa cha maziwa ya nyati.
Aidha, chembe hizo zina nguvu mara nne kushinda maziwa ya ng’ombe.
“Ni chakula kamili, unapata protini, mafuta na sukari,” amenukuliwa mmoja wa watafiti waliohusika, Sanchari Banerjee, na gazeti la The Times of India.
Mende huliwa katika maeneo mengi duniani hasa Mashariki ya Mbali
Matokeo ya utafiti huo yamechapishwa kwenye Jarida la Kimatibabu la International Union of Crystallography.
Ramaswamy anasema kwa kutumia ufahamu wao wa muundo wa protini hizo, wanaweza kutumia hamira kuzalisha chembe kama hizo kwa wingi kwenye maabara.
Aidha anabainisha kwamba muundo wa chembe hizo unaonyesha matumaini ya kuwa zinaweza kuundwa na kutumiwa katika vidonge vya dawa.
@moodyhamza