Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.

Alihudhuria sherehe za kufuzu kwenye mji mkuu Harare.

Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.

Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.

Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.

Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kumfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungozi wa Zanu-PF na urais.

@moodyhamza