Dogo Janja: mashabiki hawapati fursa ya kukutana na mimi

Siku mbili zilizopita, Dogo Janja aliitumia account yake ya Instagram kuomba ushauri au kuambiwa chochote kile na mashabiki zake. Na sasa ameiambia Dizzim Online kuhusu sababu za yeye kufanya kiu kama hicho, ambacho ni mara chache kufanyika kwa msanii aliyefikia umbali kama yeye.

“Unajua kuna watu wengi sana wanatamani kuniuliza kitu, lakini wanakuwa hawapati fursa ya kukutana na mimi labda, so nikaamua kutoa nafasi kwa yeyote yule ili niweze kujua,” amesema. “Unajua kuna mtu mwingine ana wazo zuri na labda lingekuja kunifaa zaidi kwenye muziki wangu kwahiyo nikatoa fursa

Aidha ameongeza na kusema, “Nimejifunza mengi sana kwa siku ile ikiwemo kupigania muziki wangu, nawashukuru sana.”

Dogo Janja ni msanii wa hiphop ambaye amekua kimuziki kwenye mikono ya Madee.

Source: Dizzimonline