Mrembo na staa wa muziki wa Bongo Fleva kutoka Tanzania na hitmaker wa ngoma ya ‘Rarua’ Malaika abainisha moja ya sababu kwa baadhi ya watu kuonekana kuumizwa na kuibua maneno kuhusu maisha yake kwa sasa.
Kupitia The Playlist ya Times Fm, Malaika amesema kuwa tetesi zote zinazosambaa kuhusu maisha yake ya mahusiano ni maneno ya watu ambao hawana taarifa sahihi kuhusu mpenzi wake na maisha ya kimapenzi na kuwataja kuwa wanaibua maneno kwa nia tu ya kuchafulia tu bila ushaihi wa lolote.
“Watu wanapenda kuongea vitu vingi hasa pale wanapoona ndege yako imeamka…yaani wanapoona unaaza mafanikio ndo watu wengi kuamka. Moja ya kitu ya kitu ambacho kinawaumiza kichwa sasa hivi watu wengi ni hawafahamu Malaika anatoka na nani?” Alisema Malaika.
Hata hivyo Malaika ametajwa katika kashfa ya kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja kwa kipindi ambacho amekuwa katika ziara yake nchini Marekani.
Source: Dizzimonline