Alichosema Waziri Nape kuhusu ripoti ya kamati inayochunguza tukio la Makonda

Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo  Nape Nnauye jana March 20, 2017 alifanya ziara makao makuu ya Clouds Media Group baada kuwepo taarifa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenda kwenye kituo hicho akiwa na askari wenye silaha na kuwataka watangazaji wa Kipindi cha SHILAWADU kurusha kipindi chake.

Waziri Nape aliunda Tume ya uchunguzi ya watu watano wakiongozwa na Mkurugenzi wa Habari Maelezo na kutoa saa 24 kwa tume hiyo kuzungumza na Makonda na watu wake kisha leo March 21 iwasilishwe.

Baasa ya kuona anapigiwa simu nyingi za kuhoji hatua iliyofikiwa hadi sasa Waziri Nape ametoa majibu kupitia Account yake ya Twitter na kusema>>>’Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa!

                  Source: Millard ayo