Mwakyembe Afuta Miss Tanzania.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo amesema amepiga marufuku mashindano ya Miss Tanzania kutokana na kuendeshwa kwa ubabaishaji mkubwa.

Dk Mwakyembe amesema serikali haiwezi kuruhusu ubabaishaji huo uendelee.

“Tulikuwa na Miss Tanzania hapa, mimi nimepiga marufuku,” amesema Dk Mwakyembe. “Hatuwezi kuwa tuna waparade watoto wetu, wanafanya kazi hii wakitegemea utapata gari, anatafuta hilo gari mwaka mzima, sasa huo ni uswahili ambao mimi siwezi kuukubali nikiwa kiongozi wa hii wizara. Kwahiyo nimewakatalia wote, hakuna cha Miss Tanzania. Nataka ukitaka kuanzisha hilo shindano, nataka uniwekee hilo gari uniwekee pale ofisini uniachie na switch, zawadi ya pili ni pikipiki sita basi ziwe pale nawaambia bwana ruksa,” ameongeza.

Dk Mwakyembe amesema serikali itakutana na watu wanaoeleweka kuandaa mashindano hayo kwa uhakika wa kuwepo muendelezo na utoaji zawadi usiokuwa na chenga chenga.

“Hata tuzo za muziki, zilikuwa zinategemea baadhi ya watu, wakinuna basi hiyo tuzo haipo, hatuwezi kwenda namna hiyo.

Source: Dizzim Online.