Rapa Chid Benz amemtaka Rapa Godzillah kupunguza maneno yasiyo ya msingi kwenye nyimbo zake na badala yake afanye muziki mwepesi utakao burudisha watu na siyo kuandika kizungu kingi kinachompotezea mashabiki.
Chid amesema kwamba Godzillah alikuwa muandishi mzuri wakati anaingia kwenye game lakini kwa sasa amekuwa muandishi anayeandika vitu vingi kupitiliza kitu ambacho kinamfanya aonekane kama mtu asiyejua anataka nini kwenye uandishi wake.
“Godzilla ni muandishi mzuri sana, nyimbo zake alikuwa anajua kipi aandike kipi aache lakini siku hizi amekuwa anaandika kupita kiasi hadi kuonekana kama mtu aliyechanganyikiwa. Namshauri mdogo wangu afanye muziki mwepesi ambao kama ule alioanza nao kwani alijipatia mashabiki wengi. Pia aachane na hayo makundi ya watu wanaoimba kingereza halafu lugha yenyewe hawaijui hii inamuharibia sana”, amesema Chid Benz
Vile vile Chid ameongeza kwamba “Godzilla sasa hivi nyimbo zake za zina maneno mengi kiasi kwamba unaweza kuimba halafu ukasahau mwanzo ulikuwa unaimba nini”.
Kwa upande wa Wakazi na Billnass, Chid amewataka wasanii hao wapige kazi na kuachana na Godzilla kwani amekuwa mzungumzaji kuliko vitendo.
“Wakazi nawasiliana naye sana, nilimwambia fanya kazi achana na Godzilla anayezungumza maneno 1000 kwa dakika lakini pia Billnass nimemwambia afanye muziki wake tena awe anajisifia ndio atapata mashabiki na kufika mbali sana” Chid aliongeza.
Hivi karibuni kumekuwepo na bifu linalomuhusisha msanii Godzilla pamoja na Wakazi huku msanii Billnass akitajwa kama mtu anayempatia Zilla changamoto katika muziki wake.
Source: Udaku