Linex anamuaminia Lavalava bila hata WCB


Msanii wa Bongo Flava, Linex ambaye ni mmiliki halali kabisa wa ngoma ya Kiherehere amemzungumzia msanii chipukizi kutokea lebo ya WCB, Lavalava akida kuwa hata bila kuwa WCB angetoka tu. Mjeda amesema, “Kilichoweza kumtoa lavalava ni talent, nidhamu. Uunajua kazi yoyote inahitaji nidhamu, lazima uwe na nidhamu ili uweze kuishi kwenye muziki wako au kwenye kazi yako. So Lavalava ukitoa WCB yaani bila hiyo bado angefanya vizuri. Kwasababu ni msanii mzuri kwahiyo hana kizuizi chochote cha kuacha kutoka.”Aidha Linex alizungumzia msaada aliowahi kuutoa kwa msanii huyo anayefanya vizuri na wimbo Bora Tuachane.“Lavalava nilishajaribu kumpush nilifanya naye wimbo free, hakunilipia nauli wala kuniwekea mafuta kwenye gari, wala chochote. Nilikwenda studio nikamkuta akaniomba nimfanyie verse moja kwenye wimbo wake na sikuwa na kipingamizi kwasababu niliona wimbo ni mzuri. Na dogo ana kipaji na ngoma inaitwa Wao ipo YouTube, pia ngoma nzuri so bila WCB bado angefanya vizuri,” ameeleza msanii huyo.

Source: Dizzimonline