Nick wa Pili afafanua maana ya wimbo wa ‘Ya Kulevya’

Leo kupitia kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM wasanii wanaounda kundi la Weusi wamefunguka rasmi kuhusu maana halisi ya wimbo wao mpya wa ‘Ya kulevya’ na kusema wimbo huu unamzungumzia baba wa familia kama kiongozi aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia na si kama wengine wanavyofikiria tofauti.

 >>>“Inamzungumzia baba wa familia kama kiongozi aliyepewa dhamana ya kuiongoza familia, mama na familia imempenda sana baba, kawaida ya baba akipendwa anachukulia poa, upendo umemlevya baba anaanza kufanya mambo yasiyofaa, anakuwa mtu wa ‘totoz’au Kiki”-Nikki wa Pili

>>>”Msanii ni zao la mazingira yake tumetumia maneno yanayozunguka sasa hivi tumeyatoa kwenye ‘muktadha’ yake tumeyaleta kwenye wimbo wetu tukatoa kitu”:- Nikki wa Pili

Hata hivyo Weusi wamewaahidi mashabiki zao kuwa watawaletea Video mpya ya wimbo huo soon

Source: Millard ayo