kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM Msanii na Producer kutoka Switch Records Quick Rocka amefunguka kuhusu Producer King Luffa ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye studio zake kabla ya kuhamia studio za Wanene.
Quick Rocka alisema hapakuwa na mtu aliyekuwa anamjua King Luffa lakini alimuamini na kumpa nafasi na sasa anamtakia kila la heri.
…>>>”King Luffa alikuja Switcher miaka mitatu iliyopita hakuna aliyemjua. Nikamuamini, nikampa nafasi. Namtakia kila la heri.” – Quick Rocka.
Pamoja na hayo Quick Rocka ameizungumzia issue ya Switch Music Group na Switch Record kuwa ni vitengo viwili tofauti…>>>”Switch Music Group ni kitengo kingine mbali na Switch Record hii ni label mpya ya kuibua vipaji vipya.” – Quick Rocka.
Source: Millard ayo