Barnaba apania kuongeza madem zaidi

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, hitmaker wa wa ngoma ‘Lover boy’ na mmiliki wa lebo ya High Table Sound ‘Barnaba Elias a.k.a Barnaba’ amezingumzia nia yake ya kuongeza idadi kubwa ya akina dada.

Barnaba amewaomba wadau wazidi kumsupport ili afikie lengo lake la kusaidia wasanii wengi wachanga na wenye vipaji na kuelezea kuwa mbali na kuwasaidia wachache wa kiume ndoto yake ni kusaidia na kuongeza wasanii wengi wa kike.

“Ndoto yangu ni kuongeza mademu sana, kwasasa Gold yangu ni Mullah pekee ila mademu niko na Jojo tu pekee yake kwa hiyo everything is fine na watu waendelee kunipush na naomba wadau waniunge mkono pia” Amesema Barnaba.

Hata hivyo Barnaba mbali na kuwa na nia ya kuwasaidia wasanii wanaochikupukia ameongeza kuwa safari yake bado ni ndefu na analengo la kufika mbali zaidi ya pale ambapo baadhi wanapofikiri kuwa tayari amefanikiwa.

“Nahitaji nifike pakubwa zaidi ya pale ambapo watu wanaamini mimi nimefika. I believe in God and everything is fine kwasababu bado napambana” Ameongeza Barnaba.

Source: Dizzimonline