Rapa kutoka Tanzania anayefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Bongo Bahati Mbaya’, Yound D amefichua alikopata rasta zilizobadilisha muonekanao wake ghafla muonekano ulioonekana zaidi kwenye video ya ngoma wa wimbo wake mpya.
Akizungumzia muonekano huo mpya, Young D amesema kuwa rasta hizo zenye umri wa miaka mitano ni za ndugu yake kabisa ambaye aliamua kufanya mabadiliko ya muonekano wake ambapo aliziondoa kichwani kwake na kumshauri Young D kuzitumia.
“hizi ni rasta za ndugu yangu kabisa, zina miaka mitano ambaye alizitoa kwasababu maalum za kimajukumu…kwahiyo aliyenipa hii idea ndo alinipa hizi nywele” Alisema Young D alipokuwa kihojiwa na HZB.
Hata hivyo Young D kutokana na kuingia katika mkataba na Studio za Touch Sound chini ya Mr. T Touch ameongeza kuwa mkataba wake mpya unamhitaji kikazi sana hivyo anakosa muda wa kuwa katika maisha ya mahusiano kwasasa.
Source: Dizzimonline