HAIJAWAHI Tokea..Mvua Sababisha Maporomoko ya Mawe Tanga.


Jeshi la Polisi mkoani Tanga imefunga barabara ya kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha kufuatia eneo la Mombo mkoani Tanga kuangukiwa na maporomoko ya mawe pamoja na matope na kusababisha athari kwa baadhi ya magari

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi mkoani humo Benedict Wakuyamba  amesema, maporomoko hayo yamesababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Mkoani humo na maeneo mbalimbali nchini

“Hali ya mvua imeendelea kunyesha na kufukia barabara eneo la Mombo kutokea Dar es salaam kuelekea Arusha ambapo matope na miti vimesombwa na kukwama barabarani hali iliyokwamisha magari makubwa kwa madogo kusafiri kupitia eneo hilo..Niwaombe abiria au wananchi kwa ujumla kama hawana ulazima wa kusafiri kwenda mikoa ya Kaskazini ni vizuri wakatulia kwa siku mbili tuone hali inakwendaje kwa ajili ya usalama wao”. Alisema Kamishna Msaidizi Benedict

Source: Udaku