Diamond Na Alikiba Wabadilishana Nafasi.

Wasanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz na AliKiba wamebadilishana nafasi za kazi zao na kuoenekana kuendelea kufanya vizuri ndani ya muda wa wiki moja tangu kutoka kwa video za nyimbo zao ‘Seduce Me’ na ‘Zilipendwa’.

Diamond Platnumz akiwa ni mwenye kushirikishwa katika chorus na baadhi ya vibwagizo aliwaongoza wasanii wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi na wimbo wao ‘Zilipendwa’ huku AliKiba na wimbo wake ‘Seduce Me’ zimeonekana kupigana vikumbo wa kushika nafasi nzuri ambao Seduce Me iliyoshikilia nafasi ya kwanza (Trending) ya Mtandao wa YouTube kwa siku zisizo pungua nne kisha kuuachia nafasi wimbo wa Zilipendwa kupanda na kushika nafasi ya kwanza.

Hata hivyo ushindani huu wa ngoma hizi mbili umekuwa na chachu na mazungumzo chanya kuelekea muziki kwa kila upande wa mshabiki katika kuchagua ni wimbo upi bora kwa kila shabiki anayependa mzuki mzuri kitu ambacho kinaonesha dalili za kuwa tasnia ya muziki wa Tanzania imekuwa kwa kiasi kikubwa kulingana na homa iliyotanda kwa kipinchi cha kutoka kwa ngoma za wawili hao.

Source: DizzimOnline.