Wema sepetu amchana Harmorapa,

Wema hataki mazoea na Harmorapa, amemjibu rapper huyo asiyeishiwa vituko baada ya kudai kuwa anampenda sana na yupo tayari kutangaza ndoa.

Kwenye post ndefu aliyoiandika Wema Sepetu amemuandikia Harmorapa ujumbe mzito kwenda kwa rapper huyo,

“Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this.

Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo.

Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae.

Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO? Usidharaulishe. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but AM NOT FOR U and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako LETS STOP THERE” Amendika Wema Sepetu.

Source: Millard ayo