Majibu ya Man Fongo baada ya kunyang’anywa gari

mkali wa muziki wa singeli, Man fongo. Inadaiwa Meneja wake G Maker amemnyang’anya gari pamoja na kadi aliyomkabidhi baada ya kuvunja mkataba wao.

Soudy Kazungumza na meneja wa Man Fongo…….>>>“lile pale nilimpa mdogo wangu ajishikizeshikize kwenye hili baada ya hapo nikamwambia ushaachia haina ushemeji ushakuwa super star, kuanza kutembea na boda boda tena mmepanda mshikaki inakuwa miyeyusho, mambo yakishakuwa mazuri nirudishie ndinga langu”;-G Maker

“G maker hajaninyang’anya gari ila kachukua gari kaenda kuuza kwa sababu tulivyopiga show ya fiesta nikachukua hela kama milioni 12 akaenda kununua Alteza, akanunua kwa jina lake yeye, hatukuandikishana kimaandishi lakini ile Alteza ni hela yangu mimi”:–Man Fongo