MWANAMUZIKI Darassa Aeleza Sababu za ‘Hasara Roho’ Kutofanya Vizuri


Muimbaji Darassa hivi karibuni aliachilia wimbo wake mpya ‘Hasara Roho’ lakini inaonekana kuwa mashabiki wake hawajaupokea kama wengi waliovyotarajia.

Ingawa wimbo huu hauna tofauti kubwa na Muziki sio wengi wameonyesha kuupenda na pia haujapata mtamzamo mkubwa kupitia YouTube.

Hata hivyo akizungumza kupitia kipindi cha 255 XXL cha Clouds FM, Darassa alisema kuwa mashabiki wake wamezoea Muziki zaidi kwa kuwa alikawia kuwachilia project mpya.

“Kitu ambacho kinatokea ni wimbo wa muziki umewakaa sana na kuusikiliza sana kwa namna moja au nyingine.”

Aliendelea kusema kosa lao ni kumtegemea kuachia wimbo kama Muziki ambacho hangeweza kufanya kwani kila anapoachia nyimbo lazima iwe tofauti.

“Mimi mwenyewe nilikaa sana na huu wimbo na kuupima, nikaona kuwa ni project ambayo inafaa kufuata na ikawatosha. Kwa hiyo kwa watu kukaa na kutegemea kuwa uje wimbo kama “Muziki” hiko ndio kitu kinachorudisha sanaa yetu nyuma.”

Source: Udaku