WAREMBO Washikiana Visu Kisa Penzi la Chuz

WAREMBO wawili wanaofanya tamthiliya ya Closet Chapter, waliofahamika kwa majina moja moja ya Shugga na Kanjo, hivi karibuni walishikiana visu katika ugomvi unaotajwa kuwa ni wa kumgombea bosi wao, Jumanne Kihangala ‘Mr Chuz’.

Kwa mujibu wa chanzo chetu kilicho karibu na wasanii hao, sekeseke hilo lilitokea mwishoni mwa wiki, baada ya Shugga ambaye ni mchumba wa Chuz kumuonya Kanjo apunguze mazoea na mpenzi wake huyo.

“Ishu hiyo ilitokea wakati wapo kambini Lushoto wakiwa wanashuti, ndipo Shugga akampiga mkwara Kanjo aache kumshobokea, mwenzake naye akaja juu wakaanza kudundana hadi kushikiana visu, wakidai bora wauane wakose wote,” kilisema chanzo.

Baada ya kupata habari hizo, Za Motomoto News ilimtafuta Mr Chuz  mbaye alikiri kutokea kwa ishu hiyo na kusema kinachomponza mchumba wake ni wivu wa kupindukia alionao.

Source: Udaku