Barakah The Prince Akimbia Team Kiba

 

Msanii wa muziki, Barakah The Prince ameendelea kukosa uhuru wa kifanya kile anachokitaka kupitia mtandao wa Instagram kwa madai ya kuogopa kichambo kutoka kwa Team Kiba mtandaoni.

 

Muimbaji huyo ambaye wiki hii ametangaza kuachana na label ya RockStar4000 iliyokuwa inasimamiwa muziki wake, ameonekana kukosa amani mitandaoni kutoka na kauli ambazo amekuwa akizitoa juu ya msanii Alikiba ambaye ni mmoja kati ya Wakurugenzi wa RockStar4000.

Barakah ambaye anamiliki label ya Bana Music Entertainment, ameamua kufunga sehemu za kukomenti katika mtandao wa Instagram baada ya mashabiki ambao wanaonekana kuwa wa Team Kiba kutopendezwa na kauli za muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo, Acha Niende.

Muimbaji huyo alidai amechana na label hiyo baada ya kuona kuna mambo kadhaa yameshindwa kwenda sawa huku akishindwa kuyaweka wazi.

RockStar4000 bado hawajatoa kauli yoyote juu ya kauli ya muimbaji huyo.

Muimbaji huyo mpaka sasa ana rekodi mbaya ya kukorofishana na label kadhaa ikiwemo ya Tetemesha Entertainment ambayo ilimtambulisha kwenye muziki.

Source: Udaku