Wasafi Waungana Kwa Pamoja.

Ukizungumzia wasanii wanaofanya kazi chini ya lebo ya muziki ya WCB Wasafi Tanzania hutaacha kumtaja C.E.O wa lebo hiyo Diamond Platnumz, Rayvanny, Harmonize , ,Lavalava , Queen Darleen, Rich Mavoko na msanii wa zamani wa Yamoto Band Marombosso ‘Mbosso’ ambaye ni kipindi kirefu hajasikika katika muziki kisha zikatoka taarifa za kuwa amelamba makataba tayari kama msanii wa lebo ya Wasafi.

Tasnia ya burudani ndani ya siku chache za wiki hii imekuwa na ushindani wa kimuziki ambao kila mmoja alijitanua awezavyo kikubwa tu mashabiki wa muziki wapate burudani hali iliyoibuka mara baada ya Diamond kudondoka kwa michano huku Ray Vanny akaitumia sauti yake kuimba kiitikio katika Remix ya ngoma ‘Fresh’ yake Fid Q. Ushindani umekuwa juu zaidi kiasi cha wengi kungoja yeyote kati ya wanaotegemewa na kuhusika katika mwanga mkubwa wa kutoa wimbo ambapo hali ya hewa ilitulizwa na AliKiba kwa kuachia wimbo wake ‘Seduce Me’.

Ndani ya masaa yasiyopungua kumi huku wapenda burudani wakiendelea kufurahi kilichotoka huku baadhi yao wasiache kutoa maoni yao kutokana na wanachosikiliza kama burudani ya muziki, wasanii wa lebo ya muziki ya WCB Wasafi wamekutana katika wimbo wa pamoja unaokwenda kwa jina ‘Zilipendwa’. Wazo la wimbo ni kuyazungumzia mambo yote yaliyokuwa yakifanyika kipindi cha nyuma ambayo ukiyafanya zama za sasa utakumbushwa kuwa ni Zilipendwa.

Hata hivyo wimbo huu utawagusa vijana wa zamani na wa sasa kwakuwa unawagusa wote kwa pamoja katika aina ya uwasilishaji wa kisasa zaidi na kuyazungumzia yale yote yaliyokuwa burudani na matukio yakipendwa na wa enzi hizo.

Source: Dizzim Online.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors