Vitu 11 vilivyopigwa marufuku China, Tanzania vinatumika

Kila nchi duniani imekuwa na utaratibu wake na nyingine kufikia hatua ya kupiga marufuku baadhi ya matumizi ya vitu kulingana na ama utamaduni au kuepusha purukushani ambazo huwenda zikaziingiza kwenye matatizo makubwa.

March 18 2017 millardayo.com inakusogezea hii ambayo inahusiana na China kupiga marufuku matumizi ya mambo mengi ya kiteknolojia ya kisasa hasa matumizi ya social media.

Haya ni mambo 11 ambayo huwezi kuyakuta China.

1: Instagram

Huwezi kuipata huduma ya Instagram ambayo hutumiwa na wengi duniani popote ndani ya panapoitwa Great Firewall of China.

2: Twitter

Mtandano wa kijamii ambao hupendwa sana na viongozi wengi wa dunia Twitter nao umepigwa marufuku.

3: Google

Ukiwa China huwezi kuona matokeo ya Google search wala video za YouTube ambapo Gmail ni moja kati ya huduma zitolewazo na Google lakini umepigwa marufuku huku baadhi ya watumiaji wanaotambuliwa wanaweza kuipata huduma ya Gmail kupitia Virtual Private Network (VPN) ambayo pia huweza kuingiliwa na Great Firewall.

4: Facebook

China iliizima taa Facebook 2009 na hapaoneshi kama kuna dalili za kuziwasha tena ambapo marufuku ya kuutumia mtandao huo yanahusishwa na migomo ambayo ilizuka July 2009 baina ya Waislamu wa Uighurs na Wachina wa Han katika Jimbo la Xinjiang.

5: Snapchat

Watu wa China hawawezi kupata huduma ya Snapchat pia ambayo sasa imeyafanya makampuni ya Teknolojia ya China kuanzisha networks zao.

6: Pinterest

Pinterest ilikuwa huru kupatika China kwa miaka kadhaa na ilianza kuzuiwa March 2017, kwa mujibu wa Greatfire.org, ambayo huwezesha upatikanaji wa websites China.

7: Websites

Beijing imezuia upatikanaji wa maelfu ya websites nyingi zikiwa websites za picha na video chafu huku ikiwakataza watumiaji wa Internet kuzitembelea websites ambazo zinakikosoa Chama cha Kikomunisti.

8: Filamu za kigeni (zinazotoka nje ya nchi)

China inaruhusu filamu 34 kutoka nje ya nchi kuoneshwa kwenye kumbi za cinema kila mwaka huku filamu nyingi zinazopigwa marufuku ni zile za Hollywood ambapo uhakiki wake unakutana na mkono wa Serikali ambayo inahakikisha inaondoa sehemu zote zinazohusu Chama cha Kikomunisti.

9: E-books na video

China imepiga marufuku maudhui yote ya kidigital zikiwemo movie zinazotolewa na Apple kupitia iBooks na iTunes na huduma ya Disney video-streaming huku serikali ikipitisha sheria mpya ya kuhakiki makampuni ya kigeni kuhakiki maudhui ya online kama vile videos, games na books.

10: Casino

Beijing ilipiga marufuku kamari 1949 na hakuna casino zinazoruhusiwa China.

11: Vitabu

Mamlaka zinazohusika na Uandishi na Uchapaji China hufanya mapitio ya vitabu vyote kabla ya kuchapisha China ambapo maandiko yote yanayohusu Haki za Binadamu, Tibet au Chama cha Kikomunisti hayatakiwi na kuripoti kuhusu utajiri wa Maafisa wa China pia kumezuwiwa.

.

Set featured image

                                        Source:millard ayo