Harmonize aliulizwa na Mami baby kama ilikuwa kiki au nini baada ya kudaiwa kuachana na Wolper na ukaribu wao kurejea leo wakati anaachia wimbo wake mpya.
“kuna vitu vilitokea tukajikuta hatuko sawa lakini Mungu ndio mwenye kheri tukawa tupo pamoja tukajua kabisa kuwa hiki kitu Jack hakipendi au mimi ila sasa hivi kila kitu kinaenda sawa na Mapenzi yetu sio ya kiki, nafasi yetu kwenye jamii imefanya ionekane kuwa ni kiki nilianza naye nikiwa sina hata gari” – Harmonize.
Harmonize amemtakia kila lenye kheri msanii anayefananishwa naye Harmorapa nakusema…>>> Ukiona mtu anatumia nafasi yako kuvuma ni jambo la kumshukuru Mungu, sikatai yupo kwenye miahangaiko atatoka, Mungu amjalie najua wote tunatoka kwenye familia za kimaskini ni wakati wake sasa kuonyesha alichojaliwa”:-Hamornize
Source:millard ayo