UTAFITI: Bangi kutumika kutibu saratani, kifafa na yabisi Uingereza

Kadiri maisha yanavyosogea mbele ndivyo dunia inavyokabiliana na ongezeko la magonjwa mbalimbali huku watafiti wakiendelea kutafuta namna ya kuyapunguza au kuyamaliza kabisa kwa kutafuta tiba za magonjwa hayo.

Leo March 21, 2017, nimekutana na hii ambayo unaambiwa Watafiti kutoka Oxford University, Uingereza wamezindua mpango wa kufanya Utafiti ambao utagharimu pound 10 million ambazo ni zaidi ya Tsh. bilioni 25 kujua faida za kimatibabu zitokanazo na bangi kwa ajili ya kutibu maumivu, saratani na magonjwa chochezi.

Utafiti huo unafuatiwa na ombi la baadhi ya Wabunge kupitisha sheria itakayoruhusu matumizi ya bangi kama tiba ambapo tafiti mbalimbali zimefanywa katika miaka ya karibuni ambazo zinaunga mkono thamani ya tiba itokanayo na bangi katika kutibu Parkinson, kifafa, yabisi na maumivu ya neva.

Utafiti huo umepewa jina la ‘Cannabis Research Plan’ na utafanywa kwa ushirika baina ya Oxford University na kampuni ya Kingsley Capital Partners ambayo inawekeza pound 10 million kwenye mradi huo ambapo licha ya watafiti hao kuzindua mradi huo bangi inatajwa kusababisha matatizo ya afya ya akili na imepigwa marufuku Uingereza ambapo mtu atakayekamatwa akiitumia kinyume cha sheria adhabu yake ni kifungo cha miaka mitano gerezani.

“Tatizo la kuvuta bangi ni kwamba inahusishwa na athari hasi, hivyo, kama utavuta bangi ukiwa mdogo kutakuwa na ongezeko la hatari ya kukuza matatizo kama dhiki. Tunachojua ni kuwa kuna cannabinoids kutoka kwenye mmea na mwili ambayo ina athari chanya.”

“Hivyo, lengo la utafiti huu ni kujaribu na kuondoa cannabinoids zote ambazo zina faida lakini hazina hatari ya matatizo ya akili.” – Dr Cadeer  

Source:Millard ayo