Mwanaume Ukiwa Unafanya Haya Usilalamike kwa Mkeo

 

Ikifikia mke kukusaliti kwanza unahitaji kujiuliza kuna tatizo gani mpaka akafikia kukusaliti? Mwanamke anaekupenda sio rahisi kumsaliti ampendae hata akitongozwa na Sharobaro, Mzee Yussuf, Diamond hata Reginal Mengi.

Ikitokea mkeo kakusaliti kuna kitu nyuma ya pazia lako, ingawa wengi wetu tunasema hela na Gari vinawalainisha wanawake. Wengi waliosalitiwa basi hizi ndio kasoro zao:-

1 Kaowa mwanamke wa mtu (mwanamke alikuwa na mpenzi wake lakini jamaa kaingia wakati mwanamke anatamani ndoa)

2 Alikuwa na hela sasa kafulia hana kitu au alijifanya alikuwa na hela lakini baada ya kuowa mke anagutuka mume mchovu.

3 Humtoshelezi kwenye tendo la ndoa( humkojozi) kama umeowa mke ameshawahi kufikishwa kilima cha kilimanjaro pole yako fanya maujuzi umpeleke kilima cha Everest.

4 Ubahili hapa wengi wa wanaume ndio hupigiwa sana wake zao, mke anahitaji matumizi yake binafsi sio kula na kulala tu au kumnunulia madira na chocolate za kichina. kuna matozi wanahonga mpaka malaki na milioni halafu unawacha hela ya ugali unapikiwa pilau ukimaliza kula unakwenda kulala, bwege kama wewe lazima uchapiwe dadeki zako.

5 Huna muda wa maongezi na mkeo hujui hata nini anapenda,nini leo kimemkuta,wala huna future plan kwenye familia wewe ukali,mpira,vijiwe,kazi na marafiki tuu wakati rafiki yako wa kweli(mkeo) huna muda wa maongezi nae.

6 Kuwaachia marafiki kuzoweana sana na shemegi yao, sio kama vibaya kutaniana na shemegi yao lakini kuna mataani mengine hupitiliza. utakuta mpaka baadhi ya rafiki wanampigia simu shemegi yao wanaongea kwa masaa na vicheke kibao.

7 Kujifanya mkali kila wakati wewe uso umeukunja kama ngozi za pumb..u hujulikani kijana au mzee hujulikani leo umefurahi au umenuna. Tokea umuowe mkeo hujawahi kumtania hata siku moja.

8 Kuchepuka kuna baadhi ya wanaume walioowa nishawahi kuwauliza kwanini wanachepuka jibu lao kubwa wanasema hawajui. HUbaki kumalizia kusema eti hawa wanawake watakuwa na sumaku

Kuna baadhi ya mambo husababisha sisi wenyewe wake zetu kufikia kuchukua uamuzi wa kutusaliti, Kama ukali unafanya kazi mbona simba na ukali wake lakini kazungukwa na mabebez kibao.

Source: Udaku