Ommy Dimpoz anahitaji kufanyiwa upasuaji.

 

Fresh kutoka kusanishwa na label ya Rockstar4000 na kuachia ngoma yake mpya, Cheche, Ommy Dimpoz ameshare nasi habari mbaya. Akiongea kwenye kipindi cha Chill na Sky, Ommy amesema analazimika kwenda kufanyiwa upasuaji kooni.

“Nina tatizo kwenye koo natakiwa niende kufanyiwa operation,” amesema. “Kwenye njia yangu ya kupitisha chakula kidogo mfumo wake unasumbua kwamba mpaka utanuliwe kidogo,” ameongeza.

“Lakini watu wasitishike sana, ni matatizo ambayo yanatibika halafu hayaathiri sauti, sio voice cord maake hii ndio biashara yangu na niliogopa kidogo mwanzo. So pale [Dubai] pia nilipata specialist ambaye anadeal na mambo ya ‘Esophagus’, mambo ya koo na nini.”

Tunamuombea Ommy Dimpoz alitatue haraka na salama tatizo hilo.

Source: Dizzim online.