akijitokeza mwanaume mwenye sifa hizi ntampa moyo wangu – Shilole

Shilole kama wasemavyo wazungu, ‘she is single, and ready to mingle.’ Nafasi za kuukamata moyo wake ziko wazi, lakini vigezo na masharti kuzingatiwa.

“Niko free sasa hivi, niko alone and ready to mingle,” Shishi Trump alisema kwenye Chill na Sky. “Wakiwa na vigezo ambavyo navitaka mimi niko tayari kuolewa, mimi ni mwanamke lazima niolewe. Na nilisema nikiolewa lazima niolewe juu ya ndege, hiyo ndio wish yangu kabisa,” aliongeza.

“Sasa ni lazima awe na uwezo, mambo ya ndege lazima uwe na hela. At least awe na uwezo wa kunihudumia ina maana atatoa nitatoa, kama kuna milioni 50 naye atoe milioni 50.”

Kwa upande mwingine Shilole amekiri kuwa kitu ambacho ex wake Nuh Mziwanda alimuambukiza, ni kupenda kujichora tattoo.

Source: Dizzimonline