Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini Tanzania P-Funk Majani amefunguka na kuweka wazi sababu za yeye kutoa nguvu kubwa kwenye uwekezaji kwa Wasanii wachanga ambao wanachipukia kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva.
Akiongea na DizzimOnline Majani amesema anaamini sana kwenye vipaji vya wasanii wachanga ambao anaamini kuwa umri wao utawafanya waendane na rika husika pia ni rahisi kuishi nao kwa muda mrefu.
Source: Dizzimonline