Na wewe zilikufikia taarifa za Chege kuzushiwa kifo

 

 

 

 

 

 

Mwimbaji maarufu wa Bongofleva kutoka kwenye kundi la TMK Family Chege ameeleza kwa masikitiko makubwa kuhusu taarifa za kuzushiwa kifo kupitia kwenye mtandao ambapo taarifa hizo zilisema amepata ajali mbaya ya gari na kufariki dunia.

Chege ameelezea hisia zake za masikitiko kwenye account yake ya Instagram>>>

 

Sidhani kama ni vema kuendelea kuombeana mabaya kila siku kwa kitu ambacho kina julikana na nilisha kitolea ufafanuzi kwamba hii pic ilikua ni movie tena zamani kabisa miaka zaidi ya minne ilopita kuendelea kutangaziana mabaya,Mungu anawaona na mbaya zaidi huwa analipa hapa hapa duniani,mimi sijapata ajali yoyote ndugu zangu,kusoma hamjui hata picha hamuoni?nimebadili nywele zangu muda sasa lkn napataje ajali na nywele hizo?sio vizuri,tuitumie mitandao yetu vizuri aisee,ndio maana mh magufuli aliwahi sema anatamani atokee malaika azime mitandao yote ni sababu ya watu wasio jua kwanini wapo kwenye mitandao, Mimi niko fresh kabisa lkn watu wenye haraka na wenye tamaa ya followers nawaomba msiwe wepesi wa kuandikiana mabaya,Mungu hapendi

Source: Millard ayo