Mwili wa Watekaji Watoto Arusha Wasusisiwa.


Mwili wa mtuhumiwa aliyedaiwa kuhusika na matukio ya utekaji watoto katika jiji la Arusha, Samson Petro (28) ambaye alifariki baada ya kupigwa risasi na polisi Septemba 7 mwaka huu unatarajiwa kuzikwa na jiji baada ya kutelekezwa na ndugu zake.

mhudumu wa chumba cha kuhifadhi miili katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Fransis Costa amesema tangu mwili huo ukabidhiwe na polisi hakuna ndugu aliyejitokeza.

Costa amesema baada ya mwili huo kuhifadhiwa tangu Septemba 7 sasa wanatarajia kuwapa jiji la Arusha ili wauzike.

“Kwa utaratibu wetu mwili unapokosa watu wa kuzika tunatoa taarifa jiji ili uzikwe,” amesema.

Petro ilidaiwa kuwateka na kuwaua watoto wawili, Ikram Salim(3) na Moureen David(6) wakazi wa Arusha

Source: Udaku.

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors