Je,Ni mwanamke yupi aliyekuwa na heshima zaidi? Subhannah Allaah(Mungu)

Ndugu zangu katika Imani, Mwanamke anapaswa ajifunze sharti la vazi la Hijabu kuwa ni :-

(i) Avae Jilbaab lisitiri kiwiliwili chote cha mwanamke, (pamoja na khilafu iliyopo kati ya wanachuoni kuhusu suala la uwajibu wa kuufunika uso na kutoufunika)

(ii) Jilbaab la mwanamke lisiwe na mapambo

(iii) Kitambaa cha Jilbaab kinatakiwa kiwe kizito (kisioneshe vazi la ndani)

(iv) Jilbaab linatakiwa liwe pana (lisibane)

(v) Jilbaab halitakiwi kutiwa manukato

(vi) Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya kiume

(vii) Jilbaab halitakiwi lifanane na mavazi ya makafiri

(viii) Jilbaab halitakiwi liwe ni katika mavazi ya fakhari.
Na Allaah anajua zaidi

Ndugu zangu Mwili wa mwanamke ni thamani ambayo inapasa kuhifadhiwa na kufichwa ili isipotee thamani yake. Mfano wake ni kama lulu katika kombe ambayo imehifadhika humo.

Ndugu zangu katika Imani, Mwanamke ambaye havai vazi la Hijaab, anayejipamba na kudhihirisha mapambo yake mbele ya wasiokuwa mahram wake, anakusanya madhambi mengi kwa kuwatamanisha wanaume wenye nyoyo za matamanio.
Soma Suraatil Al-Ahzaab Aya ya 32-33 kwa maelezo zaidi.

Ndugu zangu katika Imani, Wenye majukumu juu ya wanawake; mume, baba, kaka na kadhalika.

Sisi wanaume tunapaswa kuwahimiza na kuhakikisha kuwa wanawake wanavaa vazi la Hijaab, kwani wasipofanya hivyo watakuja kuulizwa kuhusu jukumu na amana yao waliyopewa kuichunga.

Wanawake wasiovaa Hijaab wanadhania kwamba wako katika maendeleo na kuwadharau wanaovaa Hijaab, na ilhali ni kinyume chake, kwamba wanaovaa vazi la Hijaab wana hadhi zaidi kuliko wasiovaa mbele ya watu na zaidi mbele ya Allaah (سبحانه وتعالى). Je, yupi aliyekuwa na heshima zaidi?
Subhannah Allaah

Enyi Ndugu zangu, Makatazo kwa wanawake wanaovaa nguo za wazi mno maharusini kwa kisingizio kuwa wako mbele ya wanawake wenziwao. Hivyo, wanafikia kuvaa nguo za kudhihirisha sehemu za mwili na hali mipaka yake ni kuonyesha sehemu ambazo huwa wazi wanapokuwa wakifanya kazi za nyumba majumbani mwao kama uso, nywele, shingo, mikono na miguu. Hivyo ni kwa sababu sehemu hizo pia ndio sehemu zinazovaliwa mapambo ya wanawake kama herini, vidani, bangili, vikufu vya miguu.

Ndugu zangu katika Imani nawaombea wanawake watimize Amri hii ya kuvaa Hijabu

story@moodyhamza