: Harmonize achukizwa na maneno ya Idris Sultan kuhusu muziki wake

 kupitia U-heard ya Clouds FM mtangazaji Soudy Brouwn ametuletea hii inayowahusu msanii wa Bongo fleva Harmonize na mchekeshaji Idris Sultan ambao wameingia kwenye mzozo baada ya kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii.

Soudy Brown amepiga story na Harmonize ili kujua kinachoendela baina ya wawili hao …>>>”Sina ushikaji na Idris, sina ushikaji naye na hatujawahi kukutana. Halafu kama sijawahi kukutania hata siku moja inakuwaje wewe unitanie?’

“Halafu nitanie vitu vingine ila usitanie muziki wangu. Tuheshimiane kila mtu aendelee kutafuta riziki yake na unaweza ukachekesha kuhusu vitu vingine na watu wakaelewa siyo lazima uchekeshe kwa kutania Brand ya mtu” – Harmonize.

Source: Millard ayo