Wanasema Diamond na Alikiba hawakai pamoja, nasema kwangu watakaa’ – Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amewataka Watanzania wote kuungana kwa pamoja ili kukuza sanaa ya burudani na michezo ikiwemo kuichangia timu ya Taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’.

Waziri Mwakyembe ameishukuru Kamati ya maandalizi iliyoundwa kwa ajili ya kutoa support kwa timu hiyo kwenda kushiriki michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana Gabon na Fainali za Kombe la Dunia wakiwemo wasanii Diamond Platnumz na Alikiba.

Source: Millard ayo