Mohammed Dewji ameshinda tuzo ya CEO Bora wa Afrika 2017

Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL Group) Mohammed ‘MO’ Dewji ameshinda tuzo ya Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) Bora wa Mwaka wa Afrika 2017.

Tuzo hizo hutolewa na Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji Afrika ‘Africa CEO Forum’ akiwashinda CEO wa BUA Group Abdulsamad Rabiu, CEO wa Cevital Issad Rebrab, CEO wa OTMT Investments Naguib Sawiris. Wengine aliowashinda kwenye tuzo hiyo ni CEO wa Bakhresa Group, Said Salim Awadh Bakhresa na CEO wa Econet Strive Masiyiwa.

Source:Millard ayo