Alichokiandika Rais wa Benki ya Dunia kuhusu jiji la Dar es salaam

Baada ya kuwekwa jiwe la msingi kwenye uzinduzi wa ujenzi wa barabara za juu (interchange) katika eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam March 20, 2017 kwa ufadhili wa Bank ya Dunia, Rais wa Bank hiyo Jim Yong Kim ameandika haya kuhusu jiji la Dar es Salaam na Tanzania kwa jumla.

“Kama ilivyo miji mingi ya Afrika, Dar es Salaam uliopo Tanzania unakua kwa haraka – na hivyo ni mji wenye msongamano wa magari. Suluhisho linahitajika, hivyo nilipewa heshima kujumuika na Rais John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya barabara ya juu Ubungo.

‘Sehemu hii ya miundombinu itawaunganisha watu wengi kwenye kazi na nafasi mbalimbali na kufanya safari kwa mabasi mapya ya mwendokasi. BRT imeelezwa kuwa tayari imepunguza muda wa kusafiri kwa dakika 90. Bank ya Dunia inafurahi kuunga mkono kazi zote na inaangalia mbele kusaidia kulifukia pengo la miundombinu Tanzania na kwingineko Afrika.” – Jim Yong Kim.

Source: Millard ayo