Mr blue Asema Haya Na mashabiki Zake.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Mr Blue amezungumzia jinsi ambavyo watanzania walivyoipokea ngoma yake mpya, Siwezi aliyomshirikisha JR. Mr Blue anayetokea kundi la Micharazo ameiambia Dizzim Online kuwa watanzania wengi hawapendi ngoma za kuelimisha.

“Unajua Tanzania imejaa watu namaanisha kuna watu ambao wanapenda burudani na wengi wao wanapenda nyimbo za starehe na za mapenzi na ndo zinakuwa zinauza sana, lakini kuna wachache sana ambao wamebaki wanapenda nyimbo za kuelimisha,” amesema Blue.

“Sasa kama mimi msanii sitakiwi niangalie tu pesa wakati mwingine natakiwa nielimishe jamii kwasababu jamii imenichagua mimi kama kioo so lazima tukumbushane. Lakini ki ukweli kabisa nyimbo hizi za kuelimisha watu hawazipendi sana lakini nitaendelea kuwakumbusha,” amesisitiza msanii huyo.

Siwezi ni wimbo ambao Mr Blue anamshukuru Mungu kwa mafanikio aliyompa.

Source:Dizzim online.