JE ni Kweli Mwanamuziki Dogo Janja Anatoka na Uwoya.


Mtangazaji Soudy Brown ametuletea U heard kwenye XXL ya Clouds FM ambayo inamuhusu staa wa Bongofleva Dogo Janja kudaiwa kuwa mapenzini na mwigizaji staa wa Bongomovie Irene Uwoya baada ya kudaiwa kuambatana pamoja kwenye safari ya Mwanza kuhudhuria Miss Ilemela.

Soudy Brown alimtafuta Dogo Janja lakini hakumpata hivyo akapiga stori na Madee ili aeleze chochote kuhusu issue hiyo ambapo alisema:

“Sina hizo taarifa za Uwoya labda wewe ndio unanipa taarifa hizo. Dogo Janja hajaniaga na sijui chochote kuhusu yeye na Irene. Ninavyojua mimi ni rafiki yake kama rafiki wengine. Sijawahi kuwaona pamoja, nasikia kama unavyosikia wewe. Nitazifuatilia.” – Madee.

 

Source: Udaku