Wasanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania waounda kundi la ‘Navy Kenzo’ Nahreel na Aika wameongezekana katika orodha ya wasanii watakaopanda jukwaa la #CastleLiteUnlocks, show itakato fanyika tarehe 22 Julai mwaka huu jijini Dar es salaam.
Kupiti ukurasa wa Instagram member wa kundi hilo la Navy Kenzo ‘Nahreel’ amethibitish uwepo wao katika orodha ya wakali watakaotumbuiza ambapo wameongezekana katika orodha ya wasanii kama rapa kutoka marekani Future, Diamond Platnumz na Cassper Nyovest kutoka Afrika Kusini.
Hata hivyo tarehe hiyo ya showitawakutanisha wakali hao ambao wameshajulikana rasmi katika viwanja va Leaders Club vilivyopo jijini Dar es salaam.
Source: Dizzimonline