Sayansi yautaja umri ambao mwanamke hufurahia zaidi mapenzi

Wengi wanaamini kuwa miaka ya 20 ndio ambayo wanawake hula raha zaidi za dunia na ndio kipindi ambacho hufurahia zaidi mapenzi aka uroda. Umri huo unafahamika wa kuyafahamu zaidi mapenzi na kukutana na mwanaume watakayempenda kwa dhati na ambapo mvuto huwa katika kilele chake huku wakiwa na nguvu ya kujirusha kabla hawajaanza kupata watoto.

Lakini, linapokuja suala la kujisikia wanavutia zaidi na kupata raha zaidi ya tendo la ndoa, umri unapoongezeka ndio huzipata raha sizizoeleka. Kwa mujibu wa utafiti mpya, wanawake hupata mapenzi bora katika maisha yao wakifikisha umri wa miaka 36 na kuendelea. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa kwa wanawake zaidi ya 2,600. Hiyo ni habari njema kwa mastaa kama akina Wema Sepetu, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper na wengine ambao wamefika ama wanaelekea katika umri huo.

Washiriki waliulizwa kuhusu namna wanavyojisikia wakifika kileleni, hisia za kuvutia na jinsi walivyofurahia tendo hilo kwenye utafiti uliofanywa na app ya Natural Cycles. Majibu yalichanganuliwa kwa makundi ya umri – wenye umri mdogo (chini ya miaka 23), katikati (23-35) na wakubwa (36 na kuendelea).

Walipoulizwa kuhusu kuvutia kimapenzi, kundi la wenye umri mkubwa lilijiamini zaidi kuhusu ngozi zao – nane kati ya 10 walisema wanajisikia kuvutia. Kinyume chake, ni wanne tu kati ya 10 katika umri wa kati walisema wanajisikia kuvutia na saba kati ya 10 walio na umri chini ya miaka 23 walisema wanafurahia muonekano wao.

Wanawake wakubwa walipata maksi zaidi katika suala la kufika kilele – karibu sita kati ya 10 waliripoti kufika kwa mshindo wa bomu ukilinganisha na watano tu kati ya 10 kwenye kundi la wenye umri wa chini. Wanawake kwenye kundi la wenye umri mkubwa wanadai kupata mapenzi bora ambapo asilimia 86 wakisema walikula uroda wa kiwango cha juu katika wiki nne zilizopita.

Hii ukilinganisha na asilimia 76 katika kundi la umri wa kati na asilimia 56 tu kwa wanawake wenye umri mdogo

Source: Dizzimonline