Davido atoa udhamini kwa mtoto aliyeimba wimbo wake

 

Muimbaji kutoka Nigeria na hitmaker wa ngoma ‘If’ Davido amechukua hatua ya kumfaidisha mtoto mmoja aliyeonekana katika video iliyochukuliwa na jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina Sham Rock na kusambaa zaidi mtandaoni akiimba wimbo wa Davido mpya wa ‘If’.

Kupitia ukurasa wa Instagram mapema jana Davido alitoa taarifa ya alichoamua kuhusu mtoto huyo aliyefahamika kwa jina la ‘Utibe’ kwa kutoa udhamini wa vitu muhimu hata kumwekea mazingira mazuri ili waweze kusoma bila tatizo la kifedha ambapo pia ametangaza kuwa tayari meshamuwekea Shilingi billion 30 kwenye akaunti ya benki.

Davido alipost ujumbe wa kuonesha kuwa aliguswa na uwezo wa mtoto huyo aliyeonekana kuujua wimbo huo kisha kuandika

“OBO GOT YOU FOR LIFE KID!!! NOTHING MAKES ME MORE THAT U FINALLY GET TO START SCHOOL!! 30 billion for ur account oooo!!!! 🙏 WE RISE BY LIFTING OTHERS!!”

Sham Rock alituma ujumbe mtandaoni wa kutamani kufanya makubwa kwa mtoto huyo ambapo aliweza kutoa mssada kidogo wa mavazi ya shule na mahitaji madogo madogo ambapo Davido alimalizia kwa msumari wa kumuandaliwa kiasi cha fedha ili aweze kusoma.

Source: Dizzimonline