TEMBO Waliovamia Udom Waondolewa.

Tembo waliovamia jana katika Chuo Kikuu cha Dodoma(Udom) na kuzua taharuki wameshaondolewa na askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa(Tanapa) ili waweze kurudi kwenye hifadhi ya Ruaha.
Akizungumza leo asubuhi, Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete amesema tembo hao wanne wameondolewa kwe maeneo hatarishi na hivi sasa askari wa Tanapa wana waswaga kuelekea hifadhi ya Ruaha.
“Askari wetu wanaendelea kuwafuatilia hivyi mpaka mchana nitatoa taarifa kamili. Ila wameshaondolewa kwenye maeneo hatarishi,”amesema Shelutete.