Mwanamke mmoja nchini India amezikata sehemu ‘nyeti’ za mwalimu wa dini katika jimbo la kusini la Keral kwa kudai kuwa alimbaka kwa miaka mingi.
Polisi wamesema kuwa mtuhumiwa anayejulikana kama Gangeshananda Theerthapada alikuwa akizuru katika nyumba ya mwanamke huyo ili kumfanyia matambiko ya ibada baba ya mwanamke huyo aliyekuwa mgonjwa.
Mama yake alikuwa na matumaini kuwa mtuhumiwa huyo aliyejidai kuwa mtakatifu ataiondolea familia hiyo matatizo. Badala yake alikuwa akimbaka msichana huyo mwenye miaka 23 kila anapotembea nyumba hiyo.
Ijumaa iliyopita alichukua kisu na kumshambulia alipojaribu kumbaka na baadaye akaita maofisa wa polisi. Mbakaji huyo alikimbizwa hospitalini ili kufanyiwa upasuaji wa dharura
Source: Udaku