Rekodi ya ushindi wa tuzo za Billboard imevunjwa na Drake

 

Usiku wa kuamkia May 22 nchini Marekani zimefanyika sherehe za utoaji tuzo kubwa za muziki na filamu, Billboard Music Awards 2017 ambapo rapa Drake ameibuka kuwa the biggest winner kwa mwaka huu.

Drake ameweka rekodi mpya kwa kushinda tuzo 13, akimuondoa star mwimbaji Adele ambaye alikuwa akishikilia rekodi ya kushinda tuzo 12 hadi kufikia May 21.

Billboards Awards imerushwa live kupitia televisheni ya ABC kutokea Las Vegas huku ikipambwa na performance za mastaa akiwemo Drake mwenyewe, Céline Dion, Cher, John Legend, Florida Georgia Line, pamoja na Lorde.

Source: Millard ayo