Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba aliendelea na ziara yake ambapo alitembelea msitu wa Amani uliopo katika Milima ya Usambara mkoani  Tanga na kujionea Ua la kipekee ambalo halipatikani sehemu nyingine duniani zaidi ya Tanzania.
Ua hilo linaitwa African Violet hustawi maeneo yenye asili ya miamba pekee limebaki moja kwa sasa katika msitu huo ambapo linasadikika kuota katika Milima ya Usambara kwa zaidi ya miaka milioni 30 iliyopita na kuwa kivutio kikubwa kwa watalii mbalimbali wanaotoka ndani na nje ya Tanzania.
Source: Millard ayo