Nandy aeleza ya Coke Studio, collabo na wasanii aliokutana nao

Mwimbaji staa wa Bongofleva Nandy anayetamba na wimbo wa ‘One Day’ yupo kwenye msimu mwingine wa Coke Studio Africa amefunguka kuhusu safari hiyo huku akiwataja pia baadhi ya wasanii aliokutana nao pamoja na mipango mingine ya kimuziki.

Akizungumza na mtangazaji Mami Baby wa Clouds FM May 21, 2017 Nandy alibainisha mambo ambayo amejifunza akisema pia kuna msanii ambaye ameomba kufanya naye collabo na amekiri pia kukutana na Nahreel.

“Nimekutana na Nahreel huku na ametutengenezea original song yetu japo ilitakiwa iwe surprise lakini nimejisikia kama nipo nyumbani kwani Navy Kenzo nimekutana nao. Hakuna msanii wa Kenya aliyeniomba collabo. kwa sababu hakukuwa na msanii kutoka Kenya.” – Nandy.

Source: Millard ayo